DER KLASSIKER-DORTMUND KUPUMZISHA MASTAA EUROPA ALHAMISI ILI KUIVAA BAYERN JUMAPILI!

 Castro: Dortmund must ignore Bayern to see out PAOK match


KOCHA wa Borussia Dortmund, Thomas Tuchel, ameamua kupumzisha Mastaa wake kadhaa kwenye Mechi yao ya Kundi lao la UEFA EUROPA LIGI ya Alhamisi ya Ugenini dhidi ya PAOKBUNDESLIGA-TEBO-SEP30 Saloniki ya Ugiriki ili wawe freshi kwa ajili ya Mtanange wa Bundesliga Jumapili na Bayern Munich.
Mechi hii, iliyobatizwa Der Klassiker huko Germany, itachezwa huko Allianz Arena na inawakutanisha Mabingwa Watetezi Bayern Munich, ambao baada ya Mechi 7, wanaongoza Bundesliga wakiwa na Pointi 21 baada ya kushinda Mechi zao zote, na Borussia Dortmund ambao wako Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 17 baada ya kushinda Mechi 5 na Sare 2.
Kwenye Mechi na PAOK Saloniki Kocha Tuchel ameamua kuwapumzisha Wachezaji Watano ambao ni Mats Hummels, Pierre-Emerick Aubameyang, Ilkay Gundogan, Sokratis Papastathopoulosa na Shinji Kagawa.
BUNDESLIGA
RATIBA
*Saa za Bongo
Ijumaa Oktoba 2
2130 Darmstadt v FSV Mainz 05
Jumamosi Oktoba 3
1630 Hertha Berlin v Hamburger SV
1630 Hannover 96 v SV Werder Bremen
1630 TSG Hoffenheim v VfB Stuttgart
1630 Borussia Monchengladbach v VfL Wolfsburg
1630 FC Ingolstadt 04 v Eintracht Frankfurt
Jumapili Oktoba 4
1630 Schalke 04 v FC Koln
1830 Bayern Munich v BV Borussia Dortmund
1830 Bayer 04 Leverkusen v FC Augsburg

About Adsense Tanzania

Zanzibar is Our Home Town, lets embrace her and enjoy her fruits while we Last.

Toa Maoni kupitia Face book / Comment Using Using Facebook

Hakuna maoni:

Leave a Reply


Top